Breaking


Jumanne, 12 Agosti 2025

CHAUMMA YAAHIDI KULETA MAENDELEO YA KIUCHUMI


 CHAMA cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimekuwa chama cha 11 kuchukua fomu ya uteuzi kugombea nafasi ya Urais na Makamu wa Rais,huku kikisema kuwa Ilani yake ya Uchaguzi imejikita katika nguzo kuu nane zenye dhumuni la kuleta maendeleo ya kiuchumi yatakayomwezesha Mtanzania kuondokana na umaskini wa kipato. 

Mgombea Urais wa Chama hicho,Salum Mwalimu,amesema hayo agosti 12,2025,mara baada ya kuchukua fomu katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC),Jijini Dodoma, akiwa ameambatana na mgombea mwenza Devotha Minja. 

Vyama vingine vilivyochukua fomu ni Chama Cha Mapinduzi(CCM),Chama Cha Wakulima (AAFP),Chama Makini,Chama Cha NRA,Chama Cha NLD, Chama cha UPDP.,Chama cha Ada Tadea ,chama cha TLP,Chama cha UMD,ambapo mwisho wa zoezi la kuchukua na kurudisha fomu kwa Tanzania Bara ni Agosti 27.

Hakuna maoni: