Breaking


Jumanne, 12 Agosti 2025

SERIKALI YATENGA MAENEO 34 KWA UWEKEZAJI WA VIWANDA NCHINI

Serikali  imetenga maeneo 34 nchini kwa ajili ya uwekezaji katika Maeneo Maalum ya Kiuchumi, hasa kwa ajili ya ujenzi wa mitaa ya viwanda, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa dira ya maendeleo inayolenga kuimarisha sekta ya viwanda.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Maeneo Maalum ya Kiuchumi na Mamlaka ya TISEZA, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, amesema serikali imeweka vigezo vitano muhimu vitakavyozingatiwa katika kuchagua wawekezaji katika maeneo hayo ikiwemo  yenye kuleta ajira nyingi Kwa vijana.

Aidha Profesa Mkumbo  ameeeza kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha maeneo haya yanatumika kikamilifu kuharakisha maendeleo ya viwanda, na hivyo kutekeleza kwa vitendo azma ya Tanzania ya kuwa taifa la uchumi wa viwanda.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA), Gilead Teri, amesema mazingira ya uwekezaji nchini yameboreshwa kwa kiasi kikubwa, na kwamba sasa kuna urahisi mkubwa kwa wafanyabiashara na wanaoagiza mizigo kutoka nje kuanzisha viwanda nchini.

Hakuna maoni: