Breaking


Jumamosi, 23 Agosti 2025

CIARA AFUNGUKA FURAHA YAKE KUHUSU USHIRIKIANO NA DIAMOND PLATNUMZ KATIKA WIMBO WA ‘LOW’


Staa wa muziki kutoka Marekani, Ciara, amegusia furaha na heshima yake ya kufanya kazi na nyota maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, katika wimbo wao uitwao “Low”, wakati wa mahojiano maalum na The Breakfast Club.


Katika mazungumzo hayo, Ciara ameweka wazi kuwa wimbo huo ni moja ya nyimbo mpya zitakazopatikana kwenye Deluxe Edition ya albamu yake ya hivi karibuni “CiCi”, ambayo itatolewa rasmi siku ya Jumatatu, Agosti 25, 2025. Albamu ya kawaida ilizinduliwa tayari tarehe 22 Agosti 2025 kama sehemu ya uzinduzi wake rasmi. 

Akielezea hisia zake, Ciara alieleza kwamba anajiona ni mtu mwenye baraka kufanya kazi na Diamond Platnumz, akiamini ushirikiano huo utaongeza mafanikio ya mradi mzima wa muziki na kufungua milango mipya kwa mradi wake wa albamu na kiutendaji. 

Ushirikiano huu, anasema, unaonyesha jinsi muziki unavyoweza kuvuka mipaka na kuleta urafiki wa kimataifa. 


Hakuna maoni: