Kamishna wa Polisi Jamii Nchini CP. Faustine Shilogile amewasili Mkoani Arusha leo Agosti 21, 2025 kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine atakutana na kuzungumza na Wakuu wa Polisi wilaya, Wakuu wa Polisi Jamii wilaya, Watendaji wa Madawati ya Jinsia na Watoto na Wakaguzi Kata wote lengo likiwa ni kuboresha utendaji wa kazi.
Katika ziara hiyo Kamishna Shilogile ameambatana na Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Makao makuu ya Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Faidha Suleiman na Mrakibu wa Polisi SP. Dkt. Ezekiel Kyogo kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni