Inauma lakini haina jinsi ndio football inamatokeo yake hasa ikiwa mojawapo hilo tuliyokutana nalo Watanzania leo kupitia mechi yetu ya robo fainali dhidi ya Morocco ambayo tumepoteza kwakufungwa bao 1-0 na kuondoshwa katika michuano ya CHAN 2024 na ikiwa ni wenyeji tukisaidiana na Kenya na Uganda.
Sasa rasmi wenyeji wawili wa michuano ya CHAN 2024 Kenya na Tanzania zote kwa pamoja zikiondoshwa leo kwenye michuano hiyo. Timu ya taifa ya Kenya wao waliondoshwa maepema dhidi ya timu Madagascar kwa penalty 4-3 baada ya sare ya bao 1-1 kwenye muda wa ziada (ExtraTime),wakati kwa timu ya Tanzania (Taifa Stars) tukiondoshwa na Morocco kwakufungwa bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa na ndio ambavyo Kenya na wao wameondoshwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Moi Kasarani.
Kwa tafsiri hiyo aliyebakia ni mwenyeji Uganda peke yake ambaye na yeye atacheza kesho dhidi ya bingwa mtetezi wa michuano timu ya taifa ya Senegal katika mchezo wa robo fainali kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Mandela mjini Kampala,Uganda.
FT: TANZANIA 🇹🇿 0-1 MOROCCO 🇲🇦
⚽️ Oussama Lamlioui 65'
#Anoldmathiasi255✍🏾

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni