Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kongwa, Mkoani Dodoma kimetangaza kuanza tena mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kongwa.
Uamuzi huo ni kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Ndugai kilichotokea Agosti 6, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Wilaya ya Kongwa, Julius Lepupuma, mchakato huo unafanyika leo na fomu zitapatikana Ofisi ya CCM Wilaya ya Kongwa na zitatolewa na Katibu wa Wilaya.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa gharama za fomu zitaendelea kuwa kama zilivyoanishwa kwenye Kanuni za Uongozi katika Vyombo vya Dola toleo la 2025, huku ikisisitiza masharti kwa waombaji ikiwemo kuwa wanachama hai wenye akili timamu na waliolipia ada.
Upigaji wa kura za maoni uliofanyika Agosti 4 mwaka huu, Hayati Ndugai aliongoza katika kura hizo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni