Nyota wa soka duniani, Cristiano Ronaldo, amevutia hisia nyingi baada ya kumpa mpenzi wake, Georgina Rodriguez, pete ya uchumba ya almasi yenye thamani ya hadi dola milioni 5 ni sawa na takriban shilingi bilioni 12.33 za Kitanzania. Pete hiyo ya kipekee ina almasi zenye uzito wa Carats 15, ni moja ya pete za thamani kubwa na za kifahari zaidi duniani.
Ronaldo, ambaye ana utajiri wa zaidi ya dola bilioni 1, ni mchezaji tajiri zaidi na anayelipwa zaidi duniani. Pete hii ni ishara ya mapenzi yao ya kudumu na mafanikio yake makubwa katika maisha.
Georgina Rodriguez amekuwa mpenzi wa karibu wa Ronaldo kwa miaka mingi, na wawili hao wanajulikana kwa maisha yao ya kifahari, ikiwa ni pamoja na makazi ya kifahari, magari ya kisasa, na safari za kifahari za ulimwenguni kote.
Pete hii ya almasi ni ishara wazi ya dhamira ya Ronaldo na jinsi anavyothamini uhusiano wao, huku mashabiki wakifurahia kuona mapenzi yao yanavyoimarika.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni