Mkutano wa sita wa wapatanishi wa kimataifa kuhusu mkataba wa marufuku ya Plastiki unafanyika nchini Uswisi, huku wawakilishi wa visiwa wakipigania kusainiwa mkataba huo muhimu kwa vita dhidi ya uchafuzi wa mazingira.
Mwakilishi wa Sychelles inayoongoza mataifa mengine 39 ya visiwa, Angelique Pouponneau, amesema mkutano huo wa Geneva ndiyo fursa ya mwisho ya kutenda kitu sahihi kwa sayari ya dunia.
Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, Inger Andersen, amesema bado kuna masuala kadhaa yanayokwamisha kufikiwa kwa makubaliano hayo, ingawa amekiri kuwa mgogoro wa kimazingira unaosababishwa na plastiki ni mkubwa na wa hatari kwa ulimwengu.
Kati ya tani Milioni-19 na 23 za takataka za plastiki huingia kwenye mifumo ya maji ulimwenguni kila mwaka, na endapo hatua hazikuchukuliwa, Umoja wa Mataifa unasema uchafu wa plastiki utafikia asilimia 50 ya uchafu wote baharini ifikapo mwaka 2040.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni