Wakili na mwanaharakati wa haki za kijamii, Mwanaisha Mndeme, leo amejitokeza kuchukua fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia chama cha ACT-Wazalendo. Zoezi hilo limefanyika katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na limehudhuriwa na umati wa wafuasi waliomshangilia kwa hamasa kubwa.
Dhamira ya Kugombea
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Mwanaisha alisema uamuzi wake unatokana na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Kigamboni na kuhakikisha sauti yao inasikika bungeni.
Vipaumbele Vyake
Mwanaisha ameeleza kuwa vipaumbele vyake vikuu vitakuwa:
• Kuboresha barabara za Kigamboni ili kuondoa usumbufu wa muda mrefu kwa wananchi.
• Kuhakikisha huduma za vivuko zinakuwa za uhakika na nafuu, kwani maelfu ya wakazi hutegemea usafiri huo kila siku.
• Kupigania kupunguzwa kwa ada ya Daraja la Mwalimu Nyerere, akibainisha kuwa daraja hilo lilipaswa kuwa ukombozi kwa wakazi wa Kigamboni, lakini ada yake imekuwa mzigo mkubwa kwao.
Wito kwa Wananchi
Mwanaisha amewataka wakazi wa Kigamboni kushirikiana naye kupitia ACT-Wazalendo ili kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa wote.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni