Breaking


Jumamosi, 2 Agosti 2025

TANZANIA (TAIFA STARS) YAANZA NA USHINDI MICHUANO YA CHAN 2024


Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burkina Faso katika mechi ya ufunguzi ya CHAN 2024 iliyopigwa  Uwanja wa Benjamin Mkapa leo.

Mabao ya Stars yamefungwa na Abdul Suleiman Sopu aliyefunga kwa mkwaju wa penalti huku Mohammed Hussein 'Tshabalala' akipigilia msumari wa mwisho.

Stars imejihakikishia pointi tatu na kukaa kileleni mwa msimamo wa kundi B lenye timu za Taifa Stars, BurkinaFaso, Madagascar Maurtania na Afrika ya Kati.

Kesho Kenya itashuka dimbani katika mechi ya ufunguzi wa kundi A dhidi ya DR Congo kuanzi saa 9:00 jioni.


Hakuna maoni: