Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendegu amesema amewataka wafanyabiashara na wananchi wa Singida kuendelea kulipa kodi kwa hiari na kutoa taarifa za ukwepaji kwani wakwepaji ndio maadui wa maendelea yanayoonekana nchini.
Ameyasema hayo tarehe 11.09.2025 ofisini kwake alipokutana na Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Mcha Hassan Mcha aliembatana na viongozi wengine wa TRA alipotembelea ofisini kwake kwa lengo kumshukuru kwa ushirikiano anaondelea kuutoa kwa TRA katika ukusanyaji wa kodi.
Mhe. Halima amesema licha ya mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa kodi na kuweza kuvuka malengo, ofisi yake imejipanga kuhakikisha mkoa wa Singida unaendelea kupiga hatua zaidi katika ukusanyaji wa kodi ili kuingia katika mikoa mitatu bora katika kuchangia pato la taifa.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni