Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanikiwa kukamata kilo 33,077.613 za dawa za kulevya aina mbalimbali pamoja na kilo 4,553 za mbegu za bangi na kuteketeza mashamba ya bangi yenye jumla ya ekari 64, katika operesheni zilizofanyika kati ya Julai hadi Septemba 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema operesheni hizo zimehusisha pia ukamataji wa silaha mbili za moto (gobore na bastola yenye risasi 11), magari tisa (9), bajaji mbili (2) na pikipiki 26 zilizohusishwa na biashara hiyo haramu huku Jumla ya watu 940 wamekamatwa kuhusika na matukio hayo ya uhalifu.
Aidha Katika operesheni maalum iliyofanyika mtaa wa Topendane, Manzese – Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, DCEA iliwakamata watu watatu wakiwemo raia mmoja wa Lebanon wakiwa na kilo 2.443 za dawa aina ya cocaine. Dawa hizo zilitoka Brazili, kupitia Kenya na Uganda, kabla ya kuingia Tanzania kupitia njia zisizo rasmi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni