Breaking

Jumanne, 9 Septemba 2025

KOCHA ZUBERI KATWILA AONGOZA SAFARI MPYA YA GEITA GOLD FC.

Kocha mkuu wa Geita Gold FC, Zuberi Katwila, ameonekana katika picha mpya zinazodhibitisha utulivu, umakini na dhamira ya kuendeleza kikosi hicho  kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Katwila, ambaye amekuwa chachu ya nidhamu na falsafa ya ushindi, anaendelea kuimarisha maandalizi ya wachezaji ili kuhakikisha Geita Gold FC inabaki kuwa miongoni mwa timu zinazoheshimika ndani ya ligi.

Mashabiki na wapenzi wa Geita Gold FC wanaendelea kuonyesha matumaini makubwa chini ya uongozi wake, wakiamini klabu itavuna mafanikio makubwa msimu huu.


 #GeitaGoldFC #ZuberiKatwila #Mwanza 

#LigiKuuTz #ChimboLaDhahabu

Hakuna maoni: