Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) kupitia Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Miundombinu, Mhandisi Leopard Runji, imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ikiwemo ujenzi wa skimu ya Umwagiliaji Makwale, iliyopo Kyela mkoani Mbeya.
Katika ziara hiyo Mhandisi Runji ameeleza kuridhishwa na kazi inayoendelea na kumtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuongeza nguvu ili kukamilisha mradi kwa wakati.
Mhandisi Runji ameeleza kuwa mradi huo unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 20.9 za kitanzania na utekelezaji wake umefikia asilimia 60.3, huku mkandarasi akiwa tayari amelipwa asilimia 50.8 ya malipo yake.
Mhandisi Runji amemtaja mkandarasi aongeze kikosi kazi ili kutumia vizuri muda uliosalia.
Kwa upande wake, Mhandisi Macarius Mlayi kutoka kampuni ya Blue Mark, mkandarasi anayetekeleza mradi huo, alisema kazi imefikia zaidi ya asilimia 60 na tuihakikishie Serikali kupitia Tume na wananchi kuwa mradi utakamilika mwezi Desemba mwaka huu.
Amezitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni uwepo wa maji mengi katika eneo la bonde linalofanyiwa kazi, hali inayosababisha ucheleweshaji wa baadhi ya ujenzi hasa nyakati za mvua.
Baadhi ya wananchi wa eneo la Makwale akiwemo Makamu Mwenyekiti wa Skimu ya Umwagiliaji Makwale,Bruno Benedicto Mwakalyobi ameeleza matumaini waliyonayo kutokana na ujenzi wa mradi huo ukikamilika kuwa utawapa wakulima fursa ya kuzalisha mara mbili kwa mwaka bila kutegemea mvua.
Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji Makwale ukikamilika, unatarajiwa wakulima zaidi ya 20,000 hivyo kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo, kuimarisha usalama wa chakula na kufungua fursa za kiuchumi kwa wakulima wa eneo hilo na mkoa wa Mbeya kwa ujumla.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni