Breaking


Jumanne, 16 Septemba 2025

RIDHIWANI AAAHIDI UPATIKANAJI WA MAJI KWA ASILIMIA 100 CHALINZE

Mgombea ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete, amesema endapo wananchi watakipa tena chama hicho ridhaa katika uchaguzi mkuu, serikali ya CCM itahakikisha upatikanaji wa maji kwa asilimia 100 na kufikia zaidi ya kaya 300,000 ndani ya jimbo hilo.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mdaula, Chalinze, Ridhiwani amesema mpango huo utalenga kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi moja kwa moja nyumbani.

Ameeleza kati ya mwaka 2015 hadi 2020 huduma ya maji ilikuwa ikipatikana kwa asilimia 54 sawa na kaya 76,096.

Hata hivyo, kwa sasa kiwango hicho kimeongezeka na kufikia kaya 95,930, sawa na asilimia 92. 


Aidha Ridhiwani amesema katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dokts Samia Suluhu Hassan, Halmashauri ya Chalinze imeongeza makusanyo ya mapato kutoka Shilingi bilioni 9.5 hadi kufikia bilioni 22.3 fedha ambazo zimeelekezwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo jimboni humo.



Hakuna maoni: