Wakulima na wafanyabiasha wa mazao ya biashara nchini wametakiwa kujiunga na bima ya kilimo ili kujikinga na majanga yotakanayo na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo usafirishaji wa mazao.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la bima ya Taifa NIC Kaimu Abdi Mkeyenge ametoa wito huo jijini Dodoma katika hafra ya utiaji Saini wa mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya benk ya ushirika na shirika la bima la Taifa kwa kusema kuwa kutokana na majanga yatokanayo na mafuriko au ukame ni vyema wakulima na wafanyabuiashara wa mazao kujikinga na bima ya kilimo.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya ushirika Godfry Ng’urah anabainisha kuwa mkataba wa makubaliano ya coop na NIC unakwenda kuwa chachu ya mabadiliko katika mikopo ya kilimo.
Meneja wa NIC kanda ya kati Alex Sunzuguye anabainisha umuhimu wa bima ya kilimo kwa wakulima walio katika vyama vya ushirika
Mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya shirika la bima ya Taifa NIC na Coop benki katika kuwahudumia kilimo niwa miaka mitatu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni