Breaking

Alhamisi, 23 Oktoba 2025

GOLI LA MAMA LIMEFIKA 💰⚽🔥



Asante sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa zawadi ya Tsh. 15,000,000 🎉 kama pongezi kwa mabao matatu tuliyowafunga Nsingizini Hotspurs! 🙌

Timu Simba Sc imepokea zawadi ya shilingi milioni 15 kutoka kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kama pongezi kwa ushindi wa mabao matatu waliopata dhidi ya Nsingizini Hotspurs.



Zawadi hiyo, maarufu kama “Goli la Mama”, ni sehemu ya motisha anayoendelea kutoa Rais Samia kwa wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ili kuongeza hamasa na ushindani kwenye michezo ya ndani.

Wachezaji wa Simba wameonyesha furaha kubwa baada ya kupokea fedha hizo, na kumshukuru Rais Samia kwa kuthamini juhudi zao na kuendelea kuunga mkono maendeleo ya michezo nchini.


Kwa zawadi hiyo, timu ya Simba imeahidi kuendeleza morali na kuhakikisha inaendelea kufanya vizuri katika michezo ijayo.


Hakuna maoni: