Leo dunia inaadhimisha Forgive an Ex Day siku maalum ya kuachilia maumivu, chuki na kumbukumbu za mahusiano yaliyopita ili kuendelea mbele kwa amani.
Siku ya Forgive an Ex huadhimishwa kila mwaka tarehe 17 Oktoba.
Hii si siku ya kumtumia ujumbe ex wako, bali ni siku ya kujichagulia amani ndani yako mwenyewe. 💛
🔹 Utafiti wa Johns Hopkins University unaonyesha kuwa watu wanaosamehe kwa dhati hupunguza msongo wa mawazo, hasira na huzuni, huku wakiboresha afya ya akili na mwili.
Wanasema, kusamehe huleta shinikizo la damu la chini, usingizi mzuri na furaha zaidi.
Kusamehe si kusahau ni kuachilia. Ni safari ya uponyaji inayohitaji muda, uvumilivu na mipaka.
Unaweza kusamehe kimya kimya, bila kutuma ujumbe wowote muhimu ni kuruhusu moyo wako upumue na kuendelea mbele. 🌸
💬 Leo, tafakari… ni nani ambaye moyo wako bado unamshikilia?
Sio lazima umtafute, lakini msamehe, kwa ajili yako.
#ForgiveAnExDay #AmaniYaMoyo #KusameheNiNguvu



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni