Malkia wa muziki wa rap duniani, Nicki Minaj, amezua tafrani mitandaoni baada ya kuondoa akaunti yake ya Instagram bila taarifa yoyote rasmi jambo lililowaacha mashabiki wake, wanaoitwa Barbz, wakiwa katika mtafaruku wa kutafuta majibu. π³π
Mashabiki wengi wamekuwa wakichunguza kila hatua ya nyota huyo, wakijiuliza kama ni hatua ya kimkakati au ni ishara ya drama mpya. Wakati huu, Nicki amebaki hai kabisa kwenye X (zamani Twitter), akiposti ujumbe wa utani, vijembe, na maneno mazito kwa mastaa wengine. π
Katika moja ya machapisho yake, Nicki alichapisha picha ya Jay-Z akiwa amevaa wig, akimshambulia Charlamagne Tha God, na kudai kuwa Keyshia Ka’Oir, mke wa Gucci Mane, “amekuwa akijaribu kuwa mimi kwa miaka mingi.” π π½π₯
Cha kuvutia zaidi ni kwamba, hatua hii ya kufuta akaunti yake inakuja wakati akitimiza miaka sita ya ndoa yake na Kenneth Petty π jambo lililowafanya Barbz wengi kuanza kubashiri huenda kuna mambo yanayochemka chini kwa chini.
Hadi sasa, hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuhusu uamuzi huo, lakini mashabiki wamerudi kusikiliza wimbo wake wa “Barbie Tingz” ambapo Nicki aliwahi kuimba:
“Had to come off IG so they can’t stalk me.”
(Ilibidi niondoke IG ili wasiweze kunichunguza.) π¬
Je, hii ni njia ya Nicki kupumzika kidogo kutoka mitandao, au ni ujanja wa “Queen of Rap” kuamsha tena gumzo duniani? ππ
#NickiMinaj #Barbz #Entertainment #MadelemoNews #TrendingNow #QueenOfRap #CelebrityBuzz

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni