Breaking

Alhamisi, 2 Oktoba 2025

TANZANIA NA KENYA ZAKUBALIANO KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA

Tanzania na Kenya zimeondoa vikwazo vya biashara visivyo vya kiushuru vinne (4)  kati ya 14 vilivyojadiliwa katika Mkutano wa  Tisa (9) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara baina ya nchi hizo ambapo hatua hii inatimiza vikwazo 58 vilivyotatuliwa kati ya 68 vilivyokuwepo huku vikwazo 10 vilivyobakia kutatuliwa ifikapo Machi 31, 2026

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah Oktoba 1, 2025 wakati wa Mkutano huo uliofanyika Dar es Salaam ambapo nchi hizo mbili zilijadili vikwazo hivyo na kutia  saini makubaliano hayo ili  kutumiza maelekezo ya makubaliano yaliyowekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya, Mhe Dkt. William Ruto, wakati wa Ziara nchini Tanzania Oktoba 9–10, 2022 kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa Biashara’s baina ya Nchi hizo.

Aidha Dkt Abdallah amebainisha vikwazo vilivyoondolewa vikijumuisha  kuondoa kodi ya zuio kwa bia za TBL kwenda Kenya, Mihuri ya ushuru (Tax Stamps Pamoja na Ada na Tarantino usafirishaji wa Bidhaa za mifugo kutoka Kenya kutekelezwa kwa kufuata maamuzi ya Baraza la Kisekta la Fedha na Uchumi la Jumuiya yaAfrika Mashariki (EAC)  na kuondoa Bima ya COMESA kwa kuwa haihusiani na Tanzania 

Vilevile, amesema Nchi hizo zimeahidi kushirikiana katika kuhakikisha biashara kati ya Tanzania na Kenya inafanyika kwa haki, kwa kuzingatia mikataba ya EAC na  kuwasilisha masuala mapya kupitia njianza idiomatic ndani ya Mwezi mmoja baada ya Mkutano huo.

“Tumekubaliana kwamba ndani ya miezi sita, ifikapo Machi 31, vikwazo vyote vitakuwa vimekwisha na suluhu zao zitatolewa kikamilifu. Kila sekta na idara ina jukumu la kukutana na upande wa pili, kujadiliana kwa pamoja na kutafuta njia za kudumu za kuyatatua. Wataalamu pia wanashirikiana kwa karibu kusaidia wafanyabiashara kuhakikisha biashara inafanyika kwa urahisi na ufanisi.

Hakuna maoni: