Breaking

Jumatatu, 17 Novemba 2025

DRC YAIPIGA NIGERIA 4-3 KWA MIKWAJU YA PENALTI

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imezima matumaini ya Nigeria ya kufuzu Kombe la Dunia la 2026 baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti katika mchuano wa mchujo wa Afrika.


DRC na Nigeria zilitoka sare ya 1-1 baada ya muda wa nyongeza kwenye mchezo uliochezwa Rabat, na timu ya Afrika ya Kati ikashinda kwa penalti 4-3 ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki hatua ya mtoanao ya mabara utakaofanyika Mexico mwezi Machi mwaka ujao.Nigeria iko nafasi 19 juu ya DRC kwenye viwango vya FIFA na ilikuwa ikipewa nafasi kubwa kabla ya mechi. 


Hata hivyo, DRC ilijipanga vyema kwa kadri muda ulivyokwenda ikaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda.

Hakuna maoni: