Breaking

Jumatatu, 17 Novemba 2025

MAREKANI: SUDAN NI MGOGORO MKUBWA ZAIDI WA KIUTU DUNIANI


Mjumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump, kwa Afrika Massad Boulos, amesema vita vya Sudan ni "mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani”, na kuwa anatarajia kuona maendeleo ya kidiplomasia kuelekea amani.


Akizungumza na Shirika la Habari la Ufaransa AFP, mjini Doha amesema "Hasa kilichotokea El-Fasher katika wiki mbili au tatu zilizopita. Sote tumeona video hizo. Tumeona ripoti hizo.


 Ukatili huo haukubaliki kabisa. Hili lazima likome haraka sana.”Tangu kuzuka mapigano Aprili 2023, kati ya jeshi la Sudan na wapiganaji wa RSF kumetokea vifo vya makumi ya maelfu ya watu na kuwapotezea makazi karibu watu milioni 12.

Hakuna maoni: