Breaking

Ijumaa, 28 Novemba 2025

HUDUMA ZA DART ZAREJEA KATIKA AWAMU YA KWANZA KUANZIA UBUNGO TERMINAL


 Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umeanza rasmi kutoa huduma za usafiri katika awamu ya kwanza, kuanzia Ubungo Terminal kuelekea Gerezani, Kivukoni na Muhimbili.


Huduma hizo zimerejeshwa leo ikiwa ni hatua ya mwanzo baada ya miundombinu ya mfumo huo kuharibiwa tarehe 29 Oktoba 2025.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa DART, William Gatambi, amesema kuwa urejeshaji huo umefanywa baada ya tathmini ambayo imebaini maeneo salama ya kuanza kutoa huduma huku ukarabati katika vituo vilivyoathirika ukiendelea kwa awamu.


Amesema kusimamishwa kwa huduma kuliathiri kwa kiasi kikubwa wananchi waliotegemea mfumo huo wa usafiri wa uhakika, na kwamba uongozi wa DART unaendelea kufanya kazi kuurudisha mfumo mzima kikamilifu.


Gatambi ameongeza kuwa wakazi wa Dar es Salaam wanatakiwa kuendelea kuwa wavumilivu wakati jitihada za kukamilisha marekebisho zikisonga mbele.


Hakuna maoni: