Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, amewahakikishia watalii kuwa hali ya usalama katika hifadhi na vivutio vingine nchini Tanzania ni nzuri na waendelee kuja kuvinjari.
Ameyasema hayo leo Novemba 28, 2025, alipotembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambapo pia alipata fursa ya kusalimiana na watalii kutoka nchi mbalimbali duniani waliokuwa wakiingia na kutoka lango la Kreta ya Ngorongoro.
“Kwa wiki tatu tu za mwezi huu wa Novemba tumepokea watalii wa ndani na nje 152, 223 idadi inayoonesha kuwa shughuli za utalii nchini zinaendelea kama kawaida na watalii wako salama kabisa,” alisema Waziri Dkt. Ashatu.
#DestinationTanzania






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni