Baada ya mapambano ya zaidi ya miaka kumi mahakamani, rapa nyota Jay-Z hatimaye ameibuka mshindi! Kesi iliyodai kuwa yeye ni baba wa kijana Rymir Satterthwaite imetupiliwa mbali rasmi Julai 2025 baada ya upande wa mlalamikaji kuiondoa kwa hiari.
Si hayo tu Mahakama ya California pia imetupilia mbali kesi nyingine iliyofunguliwa na mlezi wa zamani wa Rymir, ikieleza kuwa haikuwa na msingi wa kisheria.
Kwa hatua hii, Jay-Z hana tena kesi yoyote kuhusu madai ya uzazi, akimaliza rasmi kipindi kirefu cha sintofahamu kilichodumu kwa zaidi ya miaka kumi.
Mashabiki wake wanasema, “Hov is finally free!” 🔥🎶
👉🏽 Burudani bado inaendelea endelea kufuatilia Madelemo News kwa matukio moto kutoka ulimwengu wa mastaa! 🌍✨


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni