Breaking

Jumanne, 11 Novemba 2025

KISWAHILI SASA NI LUGHA RASMI YA UNESCO


Nyota ya lugha ya Kiswahili imeendelea kuangaza Kimataifa baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO, kuridhia kuwa moja ya lugha zitakazotumika rasmi katika mikutano mikuu ya shirika hilo.

Kauli hiyo imetolewa katika mkutano mkuu wa 43 wa Shirika hilo uliofanyika Samarkand, Uzbekistan kuanzia Oktoba 30 na unaotarajiwa kuhitimishwa Novemba 13 mwaka 2025.

Tamko hilo la UNESCO ambalo limetolewa leo limetokana na maombi yaliyowasilishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Mabaraza ya Kiswahili Tanzania-BAKITA na BAKIZA.

Kufuatia hatua hiyo tayari Tanzania imepewa fursa ya kuwasilisha hotuba ya nchi baada ya maombi yake kuridhiwa. 

Kupitishwa kwa Kiswahili kuwa Lugha ya kazi kunafanya Lugha hiyo kuwa ya kwanza yenye asili ya Afrika kupewa hadhi hiyo, huku hatua hiyo muhimu ikitarajiwa kufungua milango mingi zaidi ya Kiswahili katika taasisi, mashirika ya Umoja wa Kikanda na Kimataifa.

Hakuna maoni: