WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemchagua Mussa Azzan Zungu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), kuwa Spika wa nane wa Bunge la 13 kwa kura 378 kati ya kura 383 zilizopigwa.
Zungu ameshinda nafasi hiyo dhidi ya wagombea wengine ambao ni Veronica Tyah wa Chama Cha National Reconstruction Alliance(NRA),aliyepata kura 0,Chrisant Nyakitita wa Democratic Party(DP),kura 0,Ndonge Said Donge wa Alliance For Africa Farms Party(AAFP),kura 1,Anitha Mgaya wa National league for Democracy(NLD),kura 1 na Amin Yange kutoka Alliance for Democratic Party(ADC),kura 0.
Akitangaza matokeo hayo Novemba 11,2025, bungeni Jijini Dodoma,Katibu wa Bunge Baraka Leornad amesema kati ya kura hizo 383 zilizopigwa,3 ziliharibika.
Zungu amekuwa bungeni kwa miaka 20 sasa akihudumu nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge mwaka 2012 hadi 2021,na naibu spika wa Bunge 2022 hadi 2025 na amefanya kazi na maspika wanne mpaka sasa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni