Breaking

Jumatano, 12 Novemba 2025

MKOA WA MARA: MAKAZI YA SERENGETI NA URITHI WA ASILI WA TANZANIA

 

Mkoa wa Mara ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Unapakana na Kenya upande wa mashariki, mikoa jirani ya Mwanza na Simiyu upande wa kusini, Arusha upande wa kusini-mashariki, hatimaye Ziwa Nyanza (au Viktoria) upande wa magharibi.

 Jina linatokana na lile la mto Mara. Eneo la mkoa ni la km2 30,150, lakini kwa asilimia 36 ni maji. Sehemu kubwa ya Hifadhi ya Wanyama ya Serengeti iko ndani ya Mkoa wa Mara. 

Idadi ya wakazi ilikuwa 2,372,015 wakati wa sensa ya mwaka 2022[1], kutoka 1,743,830 wa sensa ya mwaka 2012 [2], na 1,368,602 wa sensa ya 2002[3]. Musoma ndio makao makuu ya Mkoa.

Hakuna maoni: