Breaking

Jumatano, 12 Novemba 2025

MTANZANIA SHUJAA EMANUEL AMEKAMILISHA KUCHANGIA DAMU MARA 112 HADI LEO 🌟

Hongera sana Bwana Emanuel Isaya Umbe, mchangiaji damu wa hiari na mtumishi wa Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC), kwa kuchangia damu leo kwa mara ya 112!

Kila chupa ya damu (450ml) inaweza kuokoa maisha ya wagonjwa wazima 3 au watoto wadogo 4.

πŸ“ŒHivyo mchango wake umeokoa hadi 336 wagonjwa wazima au /kama  448 watoto wadogo!na zaidi 

🀝Tunamshukuru pia Prof. Gileard Masenga Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC, kwa kuendeleza na kulea hazina hii ya Taifa, kuhakikisha watumishi kama Emanuel wanapata nafasi ya kutoa mchango wao wa hiari.

πŸ‘‰πŸ»πŸ™πŸΌ Biblia inasema

*“Kila mmoja atupe kulingana na moyo wake… Mungu hupenda mchangiaji mwenye furaha.” – 2 Wakorintho 9:7*

πŸ‘‰πŸ»πŸ€Qur’an:

*“Mioyo yenu itapewa thawabu ikiwa mtaweza kutoa kwa wengine; Mwenyezi Mungu anapenda wema.” – Surah Al-Baqarah 2:261*

πŸ’‘ Mwito: Wakuu wa Taasisi za Serikali na Binafsi, mashirika, wadau na kila mtu mmoja mmoja—tuendeleze utamaduni wa kuhamasisha watumishi na familia zetu kuchangia damu kwa hiari, tukizingatia mfano mzuri wa Hospitali ya Kanda ya KCMC.

Emanuel Umbe ni mfano wa upendo, daraja la baraka na maisha. Tuige moyo wake na tuwe sehemu ya kuokoa maisha!

Simama °CHANGIA •πŸ“πŸ“ŒOkoa Maisha

Hakuna maoni: