Breaking

Jumamosi, 29 Novemba 2025

MWANAMUZIKI JOE THOMAS AWASILI TANZANIA KUUNG’ARISHA UTALII WA MATUKIO

 Mwimbaji nyota na mkongwe wa R&B duniani, Joe Thomas, amewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kutumbuiza katika viwanja vya Leaders Club, huku ujio wake ukipokelewa kwa shangwe na hamasa kubwa kutoka kwa wapenzi wa muziki na wadau wa utalii.

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshiriki kikamilifu katika tukio hilo kama sehemu ya mkakati wake wa kuhimiza na kukuza utalii wa matukio (MICE & Events Tourism).

 Kupitia ushirikiano na wadau pamoja na watu binafsi ndani na nje ya nchi, TTB inaendelea kuhakikisha Tanzania inang’aa kimataifa sio tu kwa vivutio vyake vya asili, bali pia kwa matukio makubwa yanayovutia wageni na kuwapa watanzania fursa ya kukutana na majina makubwa duniani.

TTB imeeleza kuwa matukio kama haya yanaongeza mwonekano wa nchi, yanakuza uchumi kupitia wageni wanaotembelea Tanzania, na yanaimarisha nafasi ya Taifa kama eneo zuri na la kipekee barani Afrika.

Ujio wa Joe Thomas unaongeza hamasa katika msimu wa matukio, huku Tanzania ikiendelea kuthibitisha kaulimbiu yake Tanzania Unforgettable.

Hakuna maoni: