Karibu kwenye Meza ya Magazeti ya leo Novemba 30, 2025. Hapa tumekusogezea muhtasari wa habari zilizobeba uzito kwenye kurasa za mbele za magazeti mbalimbali nchini. Endelea kufuatilia kwa taarifa zaidi kadri zinavyoendelea kujiri.
📰 HABARILEO JUMAPILI
- Kasi utekelezaji ahadi – Ni ahadi alizotoa Rais Samia wakati wa kampeni; matunda kuonekana ndani ya wiki tatu.
- Wakimbizi wa Burundi kutiwa uraia Tanzania – Ukurasa 7
- Kutimtim cha umeya, uenyekiti CCM leo – Ukurasa 7
- “Msikubali kushawishiwa kuingia kwenye vurugu” – Kauli ya viongozi wakiwa Ngorongoro.
- Kabudi awapa somo vijana kulinda nchi yao – Ukurasa 3
- Kilimo cha muhogo kuzalisha ajira 100,000
📰 NIPASHE JUMAPILI
- Wanao daiwa kuhamasisha maandamano wakamatwa – Jeshi la Polisi lasema halitasita kuchukua hatua za kisheria.
- Mwarobaini foleni ya malori Dar wapatikana – Maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam.
- Wananchi walia bei za vyakula zikapaa – Ukurasa 5
- DPP awaachia huru watu 607 waliotuhumiwa kwa uhaini – Ukurasa 3
- Papa Leo XIV aangia msikitini, avua viatu – Ukurasa 4
📰 MWANANCHI
- Wagombea umeya rasmi vitani CCM – Uchaguzi wa ndani wa chama wakolea katika halmashauri 184.
- Magari ya kale kubamba Kilimanjaro mwisho wa mwaka – Ukurasa 3
- Mauti ya mke yatokana na ugomvi wa simu – Mume ahukumiwa jela.
- Malezi watoto wa kambo yalivyo na changamoto – Ukurasa 13
- Mfungwa Mchina atoa ushahidi dhidi ya mkuu wa gereza – Ukurasa 5
- Chadema yamililia mbunge wa zamani Naomi Kaihula – Ukurasa 2










Hakuna maoni:
Chapisha Maoni