Breaking

Alhamisi, 27 Novemba 2025

MWEKEZAJI KUTOKA ITALIA AKUTANA NA KITUO CHA PPP

 Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP- Centre) kimefanya kikao kazi kilichoongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Uendelezaji Miradi,  Innocent Mauki, kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za serikali. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mwekezaji kutoka Green EN.IT S.P.A ya Italia,  Lauro Pagani.



Majadiliano yaliyofanyika jijini Dar es salaam, yalilenga kuchambua fursa za kuanzisha na kukuza miradi miwili ya uzalishaji wa umeme wa jua yenye uwezo wa hadi MW 100 kila mmoja, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuongeza upatikanaji wa nishati safi kupitia mfumo wa PPP. Wadau walijadiliana namna ya kuimarisha ushiriki wa sekta binafsi, kuharakisha utekelezaji wa miradi na kuchochea maendeleo ya sekta ya nishati nchini.

Hakuna maoni: