Bill Nass Aonesha Upendo Mkali kwa Nandy Hata Katika Siku Zenye Changamoto
Bill Nass amemtumia mke wake Nandy ujumbe wa heri ya kuzaliwa uliojaa upendo kupitia Snapchat, huku akiwa bado anakabiliana na changamoto za maisha yake.
“Happy Birthday mke wangu!! Dunia haina maana bila wewe kando yangu. Nakupenda sana,” ameandika Nenga .
Ujumbe huu umetokea siku chache tu baada ya duka lake la simu kuliharibiwa kwenye vurugu za uchaguzi, jambo lililosababisha ajioe Instagram na kuchagua Snapchat kushiriki hisia zake kwa utulivu.
Hii ni ishara wazi kuwa upendo unaangaza hata katika siku ngumu zaidi.❤️❤️

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni