Breaking

Jumatatu, 24 Novemba 2025

RAIS BOLA TINUBU AONGEZA IDADI YA POLISI ILI KUDHIBITI HALI YA USALAMA NCHINI NIGERIA



Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, ameidhinisha kuongeza majukumu ya kipolisi kwa walinzi wa kundi la viongozi wakuu pamoja na kuamuru maelfu ya maafisa wapya kuajiriwa, kufuatia ongezeko la changamoto za kiusalama nchini humo.


Hatua hiyo imekuja wakati Rais Tinubu akikabiliwa na shinikizo kubwa baada ya zaidi ya watu 400, wakiwemo zaidi ya wanafunzi 300, kutekwa nyara katika moja ya matukio makubwa zaidi ya utekaji katika siku za karibuni nchini Nigeria.


Wakati huohuo, serikali ya Nigeria imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu kimataifa, kufuatia kauli ya Rais wa Marekani, Donald Trump, aliyetoa onyo la uwezekano wa kuingilia kijeshi akidai kuwepo kwa mashambulizi dhidi ya Wakristo na Waislamu wenye msimamo mkali nchini humo.


Kwa mujibu wa ofisi ya Rais Tinubu, hatua ya kuongeza maafisa wa usalama imechukuliwa kutokana na upungufu mkubwa wa polisi katika maeneo mbalimbali ya nchi. Serikali imeidhinisha ajira mpya 30,000 za maafisa wa polisi ili kuimarisha ulinzi na kuongeza uwezo wa kukabiliana na tishio la uhalifu.


Hakuna maoni: