Uongozi wa kitabibu wa klabu ya Wydad umetangaza kuwa mchezaji wao, Aziz Ki, amepata jeraha la kichwa wakati wa mchezo. Baada ya tukio hilo, alipelekwa hospitalini na kufanyiwa vipimo ambavyo vimethibitisha kuwa hali yake imetengemaa.
Kwa mujibu wa taratibu za kiafya, mchezaji huyo ataendelea kuwa chini ya uangalizi maalumu kwa saa 24 kama tahadhari. Klabu ya Wydad imesema itatoa taarifa zaidi mara zitakapopatikana.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni