Napoli wamefanya mawasiliano na Manchester United kuhusu mkataba wa mkopo wa Januari kwa kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo, 20. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Mainoo pia anasakwa na klabu nyingine ya Serie A huku Roma ikihitaji mkataba wa Januari. (Soccer Italia)
Kiungo wa kati wa Newcastle na Italia Sandro Tonali anatamani sana kujiunga na AC Milan, huku Juventus pia wakivutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Corriere della Sera - In Itali)
Tonali hana kipengele cha kuachiliwa katika mkataba wake wa Newcastle na atajua mustakabali wake mwaka baada ya mwaka. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Aston Villa na England Morgan Rogers, 23, anatazamiwa kusaini mkataba mpya ambao utafanya mshahara wake kuwa zaidi ya £100,000 kwa wiki. (Mail)Bayern Munich wanawasiliana na msafara wa mlinzi wa Liverpool na Ufaransa Ibrahima Konate, 26, kuhusu uhamisho unaowezekana. (Bild - via Get German Football News)
Liverpool na Chelsea huenda wakamnunua beki wa Newcastle Mholanzi Sven Botman, 25. {Offside)
Tottenham wako tayari kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, 29, mwezi Januari kutoka klabu ya Al-Ahli ya Saudi Pro League na mkufunzi wa Spurs Thomas Frank tayari amefanya naye mazungumzo. (TeamTalks)
#ChanzoBbcswahili


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni