Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, TMA, inatabiri kuwa usiku wa leo hadi kesho, mvua na ngurumo zinatarajiwa katika maeneo ya Tabora, Katavi, Kigoma, Morogoro Kusini, Ruvuma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe.
Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga inatarajiwa kuwa na mawingu kiasi na mvua katika maeneo machache.
Kwa Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi, Mtwara na Visiwa vya Unguja na Pemba, kutakuwa na mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
TMA inatoa angalizo la vipindi vifupi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Katavi na kusini mwa Morogoro.
Upepo unatarajiwa kuvuma kutoka kaskazini mashariki kwa kasi ya kilomita 20 hadi 30 kwa saa, na bahari itakuwa na mawimbi madogo hadi makubwa kiasi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni