Breaking

Jumapili, 23 Novemba 2025

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO




 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa maeneo mbalimbali nchini, kama ifuatavyo.


Kwa mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma, pamoja na Kagera, Geita na Mwanza, kunatarajiwa mawingu kiasi na uwezekano wa kupata mvua katika maeneo machache, hususan nyakati za jioni na usiku.


Kwa Visiwa vya Unguja na Pemba, pamoja na mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam, Tanga na Pwani ikijumuisha Visiwa vya Mafia, hali ya hewa inatarajiwa kuwa ya mawingu kiasi, mvua nyepesi na ngurumo katika maeneo machache.


Kwa mikoa ya Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya, mvua nyepesi inatarajiwa kutokea katika baadhi ya maeneo, huku vipindi vya jua vikiendelea.


Kwa mikoa ya Singida na Dodoma, pamoja na Ruvuma, Lindi, Mtwara, na Manyara, Arusha na Kilimanjaro, kutakuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua siku nzima.


Kwa mikoa ya Tabora, Shinyanga, Simiyu na Mara, hali ya jua na mawingu kiasi inatarajiwa kutawala katika maeneo mengi.

Miji mingi nchini itakuwa na joto la juu kati ya 25°C hadi 33°C, na joto la chini kati ya 11°C hadi 24°C, huku nyakati za mawio na machweo zikitofautiana baina ya saa 11:55 hadi 12:55.


Hakuna maoni: