Breaking

Jumatatu, 24 Novemba 2025

WAZIRI KIJAJI KUIMARISHA UTALII MOROGORO


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), ameweka bayana dhamira ya Serikali kuimarisha na kupanua ushirikiano na Mkoa wa Morogoro katika kusimamia uhifadhi na kuendeleza rasilimali za maliasili na utalii.


Dkt. Kijaji ametoa kauli hiyo leo mara baada ya kuwasili mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi, ambapo alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Adam Malima. Ziara hiyo inalenga kutembelea na kufuatilia shughuli zinazotekelezwa na taasisi mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.


Akizungumzia msimamo wa Wizara, Dkt. Kijaji amesema Serikali itaendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi, ikiwemo ulipaji wa kifuta jasho na kifuta machozi kwa wale wanaoathiriwa na wanyamapori, ili kuhakikisha haki na ustawi wa wananchi vinawekwa mbele.


Katika ziara hiyo, Waziri Kijaji ameambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), kwa ajili ya kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa majukumu ya Wizara pamoja na kuhimiza ushirikiano na mamlaka za mikoa.


Hakuna maoni: