Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa maeneo mbalimbali nchini, kama ifuatavyo, Kigoma, Kagera, Geita na Mwanza itakuwa na mawingu kiasi na vipindi vya mvua za mara kwa mara.
Mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro inatarajiwa kuwa na mvua nyepesi na vipindi vya jua. Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na mikoa ya Singida, Dodoma, Ruvuma, Lindi na Mtwara itabaki na hali ya kawaida ya mawingu na jua.
Mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Mara, Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya inatarajiwa kuwa na mawingu kiasi huku jua likionekana vipindi vya mchana.
Upepo wa pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa, hali ya bahari ikiwa na mawimbi madogo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni