Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imetangaza ofa maalum ya tiketi za safari za ndani ya nchi katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka 2025.
Kwa mujibu wa ATCL, tiketi hizo zinauzwa kwa shilingi 99,000/= kwa safari yoyote ya ndani ya Tanzania, kwa masharti ya kununuliwa na kutumika siku hiyo hiyo pekee. Ofa hiyo inapatikana kwa idadi maalum ya tiketi.
Abiria wanaotaka kunufaika na ofa hiyo wanatakiwa kununua tiketi kupitia Air Tanzania Mobile App au tovuti rasmi ya kampuni www.airtanzania.co.tz.
Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa ATCL wa kuwazawadia wateja wake na kuimarisha huduma zake katika msimu wa sikukuu.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni