Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amefunga rasmi mafunzo ya siku tatu ya waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam huku akiwataka madiwani hao kwenda kutatua kero za Wananchi.
Akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Peacock, Mpogolo amesema mafunzo hayo yawe na tija kwa kuwatumikia wananchi katika maeneo yao.
"Ukijua shida za watu wako huwezi kuona mzigo kuhudumia watu hao, nendeni katatueni kero za Wananchi katika maeneo yenu". AlisisitizaAwali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaa Mhe. Nurdin Bilal aliwataka Madiwani hao kushirikiana na wataalamu na kuepuka migogoro ili kuweza kuleta maendeleo katika Halmashauri hiyo.
Jumla ya mada kumi zilijadiliwa katika mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Chuo cha Uongozi cha Hombolo yaliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo Madiwani hao juu ya uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni