Ujumbe wa IPU umeongozwa na Balozi Ande Filip, akiongozana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa Geneva,Uswisi Dkt. Hoyce Temu ambapo katika maelezo yake Balozi Ande amesema katika Mkutano huo, Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻.
“Tanzania ni Mwenyeji na sababu kubwa ni ushiriki na historia yake katika IPU na kikubwa zaidi ni namna wao wanavyoiona Tanzania na sisi tumewahakikishia tupo tayari kuwapa ushirikiano kufanikisha mkutano huo mkubwa wa Kihistoria.” Amesema RC Makalla.
Aidha, RC Makalla amesema Mkutano huo ni fursa kwa Wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla na ukija wakati mzuri katika kudhihirisha amani, usalama na utulivu uliopo nchini na kuaminika kwa Tanzania Kimataifa, akiwataka wananchi kujiandaa kutumia fursa za ujio wa mkutano huo kiuchumi.
Vilevile, kwa Upande wake Balozi Ande kwaniaba ya Maafisa wengine wa IPU, amesema Mkutano huo wa Kimataifa utafanyika kwa siku 6 Jijini Arusha na kulingana na ratiba, washiriki wake kutoka kote duniani watakuwa na zaidi ya siku 6 Mkoani Arusha ili kuwapa fursa ya kutembelea maeneo ya kihistoria na Vivutio vya Utalii vilivyopo Arusha na maeneo mengine ya jirani.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni