Bondia Ramadhani Mkwakwate a.k.a Sungu Mtata anatarajiwa kupanda ulingoni Desemba 26, 2025 katika Ukumbi wa Warehouse Masaki, Dar es Salaam, kupambana na bondia mwenye nguvu kutoka DRC, Regan Pacho. Mkwakwate, ambaye anaendelea na maandalizi yake Chamanzi, amesema amejiandaa kwa asilimia mia moja kuhakikisha anatoka na ushindi wa kishindo.
Wadau na mashabiki wake kutoka Chamanzi wamesema kuwa licha ya umaarufu wa mabondia wa Kongo kwenye uimbaji na kucheza, wao wamejipanga kuhakikisha siku hiyo ushindi unabaki Tanzania.
Katika siku hiyo ya Boxing on Boxing Day, mapambano mengine yatakayopamba ulingo ni pamoja na:
Hassan Mwakinyo kuwaongoza mabondia ulingoni,
Hamadi Furahisha dhidi ya Hanock Phiri kutoka Malawi,
Hassan Ndonga dhidi ya Ismail Boyka,
Ally Ngwando dhidi ya Mussa Makuka,
Issa Simba wa Kahama dhidi ya Wilson Phiri wa Malawi,
Kwa upande wa wanawake: Debora Mwenda dhidi ya Mariam Dick wa Malawi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni