Breaking

Jumanne, 16 Desemba 2025

DKT. MWAMBA ATEMBELEA JENGO JIPYA LA OFISI ZA WIZARA YA FEDHA.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, ametembelea Jengo jipya la Ofisi za Wizara ya Fedha, lililopo Mji wa Serikali-Mtumba, mkoani Dodoma, ambapo amepongeza hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo hilo la kisasa linalotarajiwa kuwa ‘State of the Art’.

Dkt. Mwamba aliongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Fedha, Bw. Lusius Mwenda na Msimamizi wa Mradi Bw. Hija Mrutu na baadhi ya viongozi wa Menejimenti ya Wizara ya Fedha, kutembelea Ofisi mbalimbali ndani ya Jengo hilo na kujionea kazi kubwa iliyofikiwa katika ujenzi wa Jengo hilo ambalo linatarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni.

Dkt. Mwamba alipongeza hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Jengo hilo na kueleza kuwa zoezi la ukamilishaji wa uwekaji wa Samani litakapo kamilika watumishi wote watahamia kwenye Jengo hilo na kwamba hivi sasa baadhi ya Idara zimehamia katika Jengo Hilo.



Alisema Ofisi alizotembelea zina utulivu wa kutosha kuweza kuwawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika mazingira bora na rafiki.

Hakuna maoni: