Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema mpaka sasa wamekuwa na msimu mzuri wa kimashindano na wanaporejea katika ligi kuu wanataka kufanya kama ambyo wamefanya katika michezo ya klabu bingwa Afrika.
Amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea katika mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate ambao utacheza kesho katika uwanja wa KMC Mwenge jijini Dar es salaam.
Kocha Pedro amesema huenda akawakosa wachezaji wawili mpka watatu amabo bado wanamajeraha na wengine wanaumwa akiwemo Diara, Pacome na Mzize ambaye anamajeha ya muda mrefu.
kuhusu Diara na Pacome wanaangalia uwezakano mkapa leo jioni kama wataweza kufanya mazoezi na timu basi watakuwa sehemu ya kikosi katika mchezo huo.
Hivyo amesema mchezo huo ni changamoto mpya kwao ambayo na ni matumaini watafanya kila mbinu kubabiliana nao ili kupata matokeo ya Ushindi.
#AnaselMacha✍🏾✍🏾


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni