Kocha wa wekundu wa msimbazi Simba Selemani Matola amesema maandalizi yamekamilika kuelekea katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambapo nia ni kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.
Matola amekiri kuwa mchezo huo kwao ni muhimu na hautakuwa rahisi kwao kupata ushindi lakini watakata kuoambana na kuapat matokeo ya ushindi.
"kwa sasa hatuangalii michezo ya kimataifa ile imeshapita lakini kwa sasa tunaangalia mchezo uliokuwa mbele yetu."
"katika mchezo huo kila timu inakuja ikiwa na lengo la ushindi hivyo huu ni mchezo mwingine na tutarajie kuwa tutakuja na mbinu na mkakati mpya katika mchezo ili matokeo ya ushindi ubaki upende wetu"
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji David Kameta "Duchu" amesema wao tayari wamefanya maandalizi na wana hari kubwa katika mchezo huo watapata matokeo ya ushindi.
#AnaselMacha✍🏾✍🏾


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni