Breaking

Jumatatu, 15 Desemba 2025

JAFO: WATUMISHI KISARAWE FANYENI KAZI KWA WELEDI NA USHIRIKIANO


Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, amewahimiza watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kufanya kazi kwa weledi, bidii na kwa kushirikiana kwa karibu na Baraza la Madiwani ili kuchochea maendeleo ya wilaya hiyo na kuboresha utoaji wa huduma za msingi kwa wananchi.

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo, ambapo amesema lengo la kikao hicho lilikuwa ni kuwashukuru kwa kazi wanazozifanya na kuwaomba waendelee kutoa ushirikiano katika kuwatumikia wananchi wa Kisarawe.

“Ni muhimu kupendana na kushirikiana kama watumishi wa Serikali. Fanyeni kazi bila kuchoka, kwa kuwa mnalipwa mshahara wakati wapo wananchi wengi bado hawana ajira. Fanyeni kazi kama ibada; mkifanya hivyo kwa moyo wote mtapata mafanikio makubwa,” amesema Dkt. Jafo.

Ameongeza kuwa watumishi wanapaswa kujiepusha na utendaji wa mazoea na badala yake wafanye kazi kwa ubunifu na uwajibikaji, huku wakiacha alama chanya katika maeneo wanayoyahudumia.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kutafuta rasilimali fedha na kuhakikisha matumizi sahihi ya fedha za miradi ili miradi hiyo iwe na tija na kuleta manufaa kwa wananchi.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Nyahori Mahumbwe, ameahidi kumpa ushirikiano Mbunge huyo katika kuwatumikia wananchi na kutekeleza ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi.

“Tupo tayari kufanya kazi mchana na usiku kuwatumikia wananchi na kutekeleza ahadi mlizozitoa wakati wa uchaguzi. Watekelezaji wa mkataba ule ni sisi watumishi wa Serikali, hivyo tutahakikisha tunashirikiana kikamilifu kutekeleza Ilani ya Uchaguzi,” amesema Mahumbwe.

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe, Aidan Kitare, amesema madiwani wapo tayari kufanya kazi kwa weledi na mshikamano katika kipindi cha miaka mitano ijayo 

Hakuna maoni: