Breaking

Jumanne, 2 Desemba 2025

MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE, 2025



Hii ni Taarifa ya Habari ikikusogezea taarifa kamili kuhusu matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne uliofanyika Oktoba 2025.


Baraza la Mitihani la Tanzania leo, tarehe 02 Desemba 2025, kupitia Mkutano wake wa 163 uliofanyika jijini Dar es Salaam, limeidhinisha na kutangaza rasmi matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne pamoja na Kidato cha Pili.


Kwa upande wa Darasa la Nne, jumla ya wanafunzi 1,633,279 walisajiliwa kufanya upimaji huo. Kati yao, Wasichana walikuwa 839,515 sawa na asilimia 51.40, huku Wavulana wakiwa 793,764 sawa na asilimia 48.60.

Wanafunzi 1,530,911 ndio waliofanya upimaji—ikiwa ni Wasichana 797,691 sawa na 95.02%, na Wavulana 733,220 sawa na 92.37%.

Wanafunzi 102,368 hawakufanya upimaji, sawa na asilimia 6.27.


Katika matokeo ya ufaulu, jumla ya wanafunzi 1,320,227 kati ya 1,530,805 wenye matokeo, wamefaulu kuendelea na Darasa la Tano mwaka 2026, ikiwa ni asilimia 86.24.

Ikilinganishwa na mwaka 2024 ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 83.34, kumekuwa na ongezeko la asilimia 2.90.


Kati ya waliofaulu:


  • Wasichana ni 699,901 sawa na 87.75%
  • Wavulana ni 620,326 sawa na 84.61%



Hayo ndiyo matokeo ya Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne kwa mwaka 2025 kama yalivyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania.




 *📚ANGALIA MATOKEO HAPA👇* 


https://cutt.ly/matokeo-ya-darasa-la-nne-2025


> 🎉SHARE KWA WENGINE




Hakuna maoni: