Benki ya NMB imeendelea kuthibitisha ubora wake katika kutoa huduma kwa wateja baada ya kuibuka mshindi wa tuzo mbili kwenye tuzo za Consumer Choice Awards za mwaka huu.
Katika hafla hiyo, NMB imetunukiwa:
- Tuzo ya Benki Bora katika kutoa mikopo rafiki, kupitia huduma maarufu ya Mshiko Fasta.
- Tuzo ya Benki Bora kwa kutoa huduma za haraka, ikionesha namna benki hiyo ilivyojidhatiti kuboresha uzoefu wa mteja.
Uwakilishi wa NMB uliongozwa na Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja, Bi. Doreen Kissoky, pamoja na timu ya wafanyakazi wa benki hiyo waliohudhuria kupokea tuzo hizo.
Kwa ushindi huu, NMB imeendelea kuonesha dhamira ya kuleta huduma nafuu, za kisasa na zenye ufanisi kwa Watanzania.
#NMBKaribuYako


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni